Jina la Mtumiaji (Username) ni barua pepe yako ambayo uliingiza wakati wa kujisajili. Endapo umesahau neno siri lako, ingiza barua pepe yako na kisha ubonyeze sehemu ya Password (Neno Siri)?
(Neno Siri) Password? Ni chaguo lililopo chini ya sehemu ya kuingilia upande wa juu kona ya kulia ya tovuti yetu.
Baada ya kuwa umeshabofya sehemu ya Neno Siri (Password)? fomu fupi itajitokeza ambayo utatakiwa kuijaza ukiwa na barua pepe yako na swali la ulinzi.
Barua pepe ikiwa na linki ya kurekebisha neno siri lako yenye uthibitisho itaingia kwenye jumbe zako za barua pepe. Mara tu baada ya kupokea ujumbe huo unapaswa kuubonyeza haraka kwa sababu linki hiyo ni ya muda mfupi tu. Utapokea neno siri la muda tu. Utakapoingia kwa kutumia neno siri hilo, tovuti yetu itakutaka ubadili neno siri lingine, ingiza neno siri hilo la muda kwenye sehemu ya neno siri la zamani, na kisha neno siri ulilopanga kutumia siku za mbeleni kwenye sehemu ya neno siri jipya.