Baada ya kuingia mtandaoni, neno siri lako la sasa linaweza kubadilishwa kwenye sehemu ya Akaunti Yangu (My Account) kwenye kijisehemu cha Kubadili Neno Siri (Change Password) upande wa kushoto.
Ingiza neno siri lako la sasa, kisha neno siri jipya na kisha uingize tena neno siri hilo jipya.
Bofya sehemu ya Kubadili Neno Siri (Change Password) ili kuhakiki badiliko lako.